103. Njoni Kwangu
Softly and Tenderly
1. Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami;
Moyoni mwetu hungoja, hukesha, Hukungojea wewe.
“Njoni kwangu, Mliochoka, njoni:
Yesu huita kwa upole mwingi, Akwita, “uje kwangu”
2. Atuombeapo usikawie, Hutuombea sisi;
Usidharau wema ma huruma, Huruma kwetu sisi.
3. Siku za maisha hupota hima, Hupita kwako, kwangu;
Usiku waja, kifo kinakuja, Huja kwako na kwangu.
4. Fikiri juu ya upendo wake, Upendo kwako, kwangu;
Dhambi zetu amekwisha samehe. Masamaha ni yetu.