104. Yesu Aliniita “Njoo”
I Heard the Voice of Jesus Say
1. Yesu aliniita, “Njoo Raha iko kwangu,
Kichwha chko ukilaze Kifuani mwangu”
Nilikwenda kwake mara, sana nilichoka;
Nikapata kwake raha Na furaha tena.
2. Yesu aliniita, “Njoo, Kwangu kuna maji;
Maji ya Uzima, bure, Unywe uwe hai.”
Nilikwenda kwake mara na maji nikanywa;
Naishi kwake na kiu Kamwe sina tena.
3. Yesu aliniita, “Njoo, Dunia i giza,
Ukinitazama, nuru Takung’arizia.’
Nili kwenda kwake mara, Yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga Safarini Mwangu.