119. Alilipa Bei
I Hear the saviour Say
1.Yesu anasema, “Wewe huna nguvu
Kesha ukaombe, Na uje, Mwanangu.
Alilipa bei, Nawiwa naye;
Dhambi ilitia waa, aliiondoa.
2. Bwana, nimeona Uwezo wako tu
Waweza ‘takasa Mioyo michafu.
3. Sina kitu chema Kudai Neema,
Hivi nitafua Mavazi kwa damu.
4. Ninaposimama Juu ya mawingu,
Taji nitaweka Miguuni pa Yesu.