(NZK # 19) MSALABANI PA MWOKOZI
1. Msalabani Pa Mwokozi, Hapo Niliomba Upozi,
Moyo Wangu Ulitakaswa, Na Asifiwe.
- Na Asifiwe,
Na Asifiwe.
Alitukomboa Kwa Damu,
Na Asifiwe.
2. Chini Ya Mti Msumbufu, Niliomba Utakatifu,
Alinikomboa Kwa Damu, Na Asifiwe.
3. Kwa Ajabu Ninaokoka, Yesu Anakaa Moyoni;
Mtini Alinifilia, Na Asifiwe.
4. Damu Ya Yesu Ya Thamani, Huniokoa Makosani;
Huniendesha Wokovuni, Na Asifiwe.
it was amazing 😍