159. Anakuja Upesi
How Sweet are the Tidings
1. Anakuja upesi, Yesu Bwana wetu, Msafiri mbali na kwao;
Alisema dhahiri, “Nitakuja tena”; Amina; na uje, E Bwana.
Yuaja, Yesu atarudi sasa; Anakuja duniani.
Wasafiri wote watapumzika Yesu anaporudi tena.
2. Makaburi yote wafu wanapolala Yatafunguliwa tena;
Na mamilioni pale wataondoka tena, Wasione machozi kamwe.
3. Hatutatengana na hao tena huko; Nyimbo nzuri tutaimba.
Watakusanyika ‘toka kila kabila, Miguuni pa Mwana-kondoo.
4. Aleluya Amin! Aleluya tena! Upendo wake unashinda!
Tutamsifu milele, hata tutashangaa, Jinsi alivyo tukomboa.