177. Kazi Yangu Ikiisha
When my Life-work is Ended
1. Kazi yangu ikisha, nami, nakiokoka,
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi; nivukapo ng’amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
Nitamjua, nitamjua,
Nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua,
Kwa alama za misumari.
2. Kuona uso wake utanipa furaha,
Furaha isiyo ya kukomesha;
Nitamsifu Mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyo nipa pahali mbingini.
3. Nao walio kufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
4. Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi awla huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele: lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.