5 – Tumwabudu Mfalme Mtukufu

0
42

(NZK # 5) NA TUMWABUDU MFALME MTUKUFU
(O Worship The King)

 1. Na Tuumwabudu Huyo Mfalme,
  Sifa Za Nguvu Zake Ziimbe;
  Ni Ngao, Ni Ngome, Yeye Milele,
  Ndizo Sifa Zake Kale Na Kale.
 2. Tazameni Ulimwengu Huu,
  Ulivyoumbwa, Ajabu Kuu;
  Sasa Umewekwa Pahali Pake,
  Hata Utimize Majira Yake.
 3. Kwa Ulinzi Wako,Kwetu Bwana,
  Twakushukuru, U Mwema Sana;
  Hupewa Chakula Kila Kiumbe,
  Kila Kitu Kina Mahali Pake.
 4. Wanadamu Tu Wanyonge Sana,
  Twakutumaini Wewe, Bwana;
  Kwamwe Haupungui Wako Wema,
  Mkombozi Wetu, Rafiki Mwema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here