(NZK # 4) Jina La Yesu, Salamu (All Hail The Power)
- Jina La Yesu, Salamu! Lisujudieni,
Ninyi Mbinguni, Hukumu, Na Enzi Mpeni.
Ninyi Mbinguni, Hukumu, Na Enzi Mpeni. - Enzi Na Apewe Kwenu, Watetea Dini;
Mtukuzeni Bwana Wenu, Na Enzi Mpeni.
Mtukuzeni Bwana Wenu, Na Enzi Mpeni. - Enyi Mbegu Za Rehema Nanyi Msifuni;
Mmeponywa Kwa Neema, Na Enzi Mpeni.
Mmeponywa Kwa Neema, Na Enzi Mpeni. - Wenye Dhambi Kumbukeni Ya Msalabani.
Kwa Furaha Msifuni, Na Enzi Mpeni.
Kwa Furaha Msifuni, Na Enzi Mpeni. - Kila Mtu Duniani Msujudieni,
Kote-Kote Msifuni, Na Enzi Mpeni.
Kote-Kote Msifuni, Na Enzi Mpeni. - Sisi Na Wao Pamoja Tu Mumo Sifani.
Milele Sifa Ni Moja, Ni “Enzi Mpeni”.
Milele Sifa Ni Moja, Ni “Enzi Mpeni”.