156 – Uniongoze, Yehova

0
61

156. Uniongoze, Yehova
Guide Me, O Thou Great Jehovah

1. Uniongoze, Yehova, Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, u hodari, ‘Nilinde kwa mkono.
Unitunze, unilinde, Unionyeshe njia!

2. Na kisima cha uzima, Maji ya utabibu,
Fungua kwa moyo wangu, Ninywe na kuponyeka!
Uninyweshe, unilishe, Hata nimetosheka.

3. Wakati wa kuuvuka, Ule mto Yordani,
Hofu yangu ufariji, ‘Nione uso wako.
Nyimbo shangwe, nyimbo shangwe, Nitaimba daima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here